Maadili Movie

Maadili Movies


Lengo ni kusimamia ulinzi wa maadili mema kupitia filamu za Kitanzania, kuazisha, kuendeleza na kuhamasisha uwepo na ukuwaji wa filamu zenye heshima, zinazozingatia maneno, matendo na mavazi yenye maadili.

nchi ya Tanzania ni nchi inayochipukia kiuchumi na kiteknologia, hivi sasa kumeibuka makampuni mengi madogo madogo yenye kujaribi kutengeneza filamu na michezo ya Luninga.

Tumeshuhudia aina mbalimbali ya ukiukwaji wa maadili na filamu zenye kwenda kinyume na utamaduni wa Mtanzania na imani zetu za dini.

Nasi ndio tukaonelea tuanzishe chombo kitakachoweza kutengeneza filamu zinazokwenda sambamba na maadili na kutunza heshima ya Mtazamaji, yeye na familia yake ili jamii iweze kuburudika na wakati huo huo kulinda heshima na maadili ya jamii.

Ukurasa huu utakuwa ukiweka habari, hoja na picha na kila linalojiri katika ulimwengu wa filamu za Kitanzania, ili msomaji aweze kujifunza na kuelimika na wakati huo huo kuburudika na filamu zenye kwenda sambamba na maadili yetu.

Karibuni sana katika ukurusa wetu huu.

1 comment:

  1. Asalam Alaykum. kwa jina naitwa WAZIRI MOHAMED MAPUNDA, kwa sasa nipo Dar es salaam Kikazi. Nimetunga Tamthiliya yenye maadili ya Kiislam na ninataka kushirikiana na waigizaji waliowahi kufanya kazi hii ili tuweze kuiigiza na kuitoa. kwa kampuni au walio tayar tuwasiliane kwenye 0759037671. au nitafute kwenye email yangu wazirimwanazuoni@gmail.com

    ReplyDelete