Tuesday 27 May 2014

MAADILI MOVIES KATIKA MTANDAO



Lengo ni kusimamia ulinzi wa maadili mema kupitia filamu za Kitanzania, kuazisha, kuendeleza na kuhamasisha uwepo na ukuwaji wa filamu zenye heshima, zinazozingatia maneno, matendo na mavazi yenye maadili.

nchi ya Tanzania ni nchi inayochipukia kiuchumi na kiteknologia, hivi sasa kumeibuka makampuni mengi madogo madogo yenye kujaribi kutengeneza filamu na michezo ya Luninga.

Tumeshuhudia aina mbalimbali ya ukiukwaji wa maadili na filamu zenye kwenda kinyume na utamaduni wa Mtanzania na imani zetu za dini.

Nasi ndio tukaonelea tuanzishe chombo kitakachoweza kutengeneza filamu zinazokwenda sambamba na maadili na kutunza heshima ya Mtazamaji, yeye na familia yake ili jamii iweze kuburudika na wakati huo huo kulinda heshima na maadili ya jamii.

Ukurasa huu utakuwa ukiweka habari, hoja na picha na kila linalojiri katika ulimwengu wa filamu za Kitanzania, ili msomaji aweze kujifunza na kuelimika na wakati huo huo kuburudika na filamu zenye kwenda sambamba na maadili yetu.

Karibuni sana katika ukurusa wetu huu.

1 comment: