Wednesday 18 June 2014

DUNIA ITAWATAMBUA

 Matron wa kundi la sanaa za maadili linalojulikana kwa jina la MASH PRODUCTION dada Sanura Omar mmoja wa washiriki katika filamu mpya ya maadili inayoitwa SIHRI
 Binti mdogo mwenye kipaji kutoka katika kundi linalofanya filamu za maadili hapa nchini MASH PRODUCTION, Samiya Abdul aliyeshiriki kama muhusika mkuu katika ya SIHRI anaeamini zaidi katika elimu maishani wakati huu ameamua kuudhihirishia ummah juu ya ukubwa wa kipaji alichonacho hakika ulimwengu utamtambua
 Munawwar Hassan
 Anaitwa Nuurat Kipati amefanya vizuri katika uimbaji wa qaswida alipotoka na albamu ya mzizima wadau walimtambua kwa mara ya kwanza alipotoka katika filamu ya yusra akiwa kama mfanyakazi katika duka kubwa la urembo linalomilikiwa na yusra ujio wake mpya ni kuwaonesha wadau kipaji kikubwa alichojaaliwa na mwenyezi utamuona tena katika filamu ya SIHRI kama mmoja wa washiriki muhimu akiiunganisha filamu katika pande zenye utata
 Hassan China wengi humuita dokta amefanya vizuri katika filamu ya yusra alipocheza kama dokta wa yusra alionekana pia katika filamu ya hadaa alionesha kipaji chake katika filamu ya nafsi lawwama ambayo inafanya vizuri mno kwa sasa huko mitaani Dr China sasa utamwona kwa uhuru katika filamu ya SIHRI  ni hazina ya vipaji na sababu ya ushindi wa maadili movies
Dada Munawar Hassan huyu ndie kila kitu katika filamu ya SIHRI ameichukua hadithi ya filamu kutoka upande mmoja na kusafiri nayo kwa ufupi anaipindua hadithi kutoka hali moja kwenda nyingine akionekana kama mama mwenye huruma na mapenzi ya kweli kwa mtoto wake Samiya aliyecheza kama Latifa katika filamu ghafla linakuja jambo linalotikisa mioyo yao hakika uwepo wake katika filamu za maadili utawasahaulisha wengi kupenda filamu zilizokosa adabu

No comments:

Post a Comment