Tuesday 1 July 2014

MCHANA PEKEE HAUKUTOSHA KUIKAMILISHA FILAMU YA SIHRI

 Director wa filamu ya SIHRI Said Kinyogoli akikuna kichwa katika kuwazua ni vipi utatumika kwa usahihi muda mchache wa usiku katika kukamilisha matukio ya usiku yanayotakiwa katika filamu ya SIHRI filamu hii kwa sasa imekamilika na iko tayari kukuburudisha na kukuelimisha katika picha kushoto ni mkuu wa sauti na mwanga katika filamu hiyo anaejulikana kwa jina la profeshino Jongo
 Director Said Kinyogoli kulia akitoa maelezo kwa wasanii vinara walioshiriki katika filamu ya SIHRI kushoto ni Suleiman Mohamed (bob sule) na ukhti Munawwar wakisikia kwa umakini maelezo hayo filamu ya SIHRI imekamilika na inasambazwa na MADRASA SHOP nchini kote ni muendelezo wa mapinduzi kutoka katika filamu zisizo na maadili mpaka ulimwengu huu wa filamu za heshima jitahidi upate nakala yako
 Hadj Mgwami kushoto (sniper) akiwa na kampuni nzima ya peace production ndio wapishi kamili wa filamu ya SIHRI kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake hakika utaalamu wa hali ya juu umetumika kuhakikisha malengo yanatimia  kulia ni wasanii maarufu wa kutoka madrasa shop bilali, fahd na bashiri wakishiriki kikamilifu katika location ya filamu hiyo hakika mcaha pekee haukutosha ililazimika muda mwingi wa usiku utumike ili kuifanya filamu iwe na kitu cha tofauti
mkurugenzi Swaleh Humoud akifuatilia simu pamoja na director said kinyogoli ili kuweka mambo sawa katika uchukuaji picha wa filamu ya SIHRI kazi ilifanyika kwa uhakika hasaaa

No comments:

Post a Comment